Use APKPure App
Get Tafakari Injili old version APK for Android
Jifunze neno la Mungu kwa njia ya Tafkari ,Maswali na Masomo mbalibali .
Hii ni app ambayo imeandaliwa mahususi kwa lengo la kusaidia mkristo kukua kiroho kupitia vipengele mbalimbali vilivyo jumuishwa ndani yake ikiwa ni pamoja na Kipengele cha :
1: Aya Za Biblia
Hapa tunapata Aya mbalimbali za Biblia zilizowekwa kwenye makundi mbalimbali kama vile Aya zinazohusu Amani,Imani, Familia,Upendo,Ahadi za Mungu,Ulinzi wa MUngu, Uvumilivu, Kushinda Hofu n.k. Yote ikiwa na lengo la kuwasaidia namna ya kusimamia neno la Mungu kulingana na halia ama changamoto wanazopitia
2: Nukuu
Maneno mbalimbali kutoka kwa walimu wa mafundisho ya neno la Mungu na kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Mungu ambayo yatatusaidia kusimama kiimani na kukuza imani yetu ndani ya Mungu katika Kristo Yesu.
3:Tafakari Fupi
Kutoka katika sura fulani ya biblia na kulingana na ROHO MTAKATIFU atakavyotuongoza tunapata tafakari ya neno la Mungu ambayo inatupa uelewa wa kina kuhusu jambo fulani katika maisha, kwa leno la kukuza imani na kutupa muongozo wa nini tufanye ili katika maisha kupendau ya Mungu.
4:Masomo
Tunatazamia kuwa na masomo yanayo husu maeneo mbalimbali katika Imani na maisha, ambayo yatakuwa na mtiririko mzuri kuanzia sehemu ya kwanza Hadi ya mwisho. Kwa mfano tunaweza kuwa na masomo yanayohusu "IMANI" , "NGUVU YA DAMU YA YESU" ,"MALANGO" , "NDOA","MALEZI NA FAMILIA "Hivyo kipengele hiki kitatoa fursa za kuelezea kwa kina somo hatakama linavipengele 7 au zaidiiwa kavyote mtiririko mzuri.
3:Aya ya siku/ujumbe wa siku
Kupitia app kila siku utakuwa unapokea Aya kutatoka sura tofauti tofauti za biblia zilizowekwa kwenye makundi mbalimbali sama vile Aya zinazohusu Amani,Imani, Familia,Upendo,Ahadi za Mungu,Ulinzi wa MUngu, Uvumilivu, Kushinda Hofu n.k. Yote ikiwa na lengo la kutiana moyo, kukumbusha ahadi a Mungu,kukumbusha maangizo ya Mungu na kwa ujumla wake kukuza Imani kama mtoto wa Mungu hasa kulinga na halifulani ya maisha ambayo mtu anapitia
Unaweza kutumia aya hizi kumshirikisha ndugu, rafiki ,jamaa na watu wengine, kuwainjilisha,kuwaongoza na kuwashauri ikiwa wapo kwenye uhitaji wa namna hiyo, tukizingatia kuwa uhitaji wetu kiroho na kimwili ni tofauti kwa kila mtu na siohandanikoi woko watu na siohandanikoi yanaweza kuwasaidia kuvuka katika changamoto mbalimbali ama kuzitumia kumshinda shetani.
4:Permainan/mchezo
Huu ni mchezo wa maswali na majibu kutoka katika sura mbalimbali za biblia , ambazo zimegawanyika katika makundi matatu,
-- Moja maswali kutoka agano jipya,
-- Pili maswali kutoka Agano la kale na
-- Tatu mchanganyiko wa Maswali kutoka Agano jipya na la Kale.
Lengo kubwa ni kuongeza uelewa na ufahamu katika kusoma biblia Kwa watoto na watu Wazima pia ambao watakuwa na swali fulani ambalo wanaweza kujibu na kupima uelewa wao katika maandiko.
5:Ujumbe kwa njia ya Sauti
--Katika kipengele hiki Tunatazamia kuwa jumbe mbalimbali za neno la Mungu na masomo vitapatikana pamoja na Nyimbo za injili ambapo watu wanaweza kusikiliza na kupakua bila shida yoyote.
6:Kipengele Cha mawasiliano
Hapa tutajikita zaidi katika masuala ya Maoni,ushauri na maswali ikiwa mtu anahitaji kufanya hivyo, Basi uwanja huu utamfaa sana.
Zab 54:4
Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
Flp 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Tuombeane dan kuitenda kazi ya Bwana.
Mungu asema: “Nitakufunza na kukuonesha njia unayopaswa kufuata. Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.
Last updated on Feb 20, 2022
Minor bug fixes and improvements. Install or update to the newest version to check it out!
Dimuat naik oleh
Kumbhar Irfan
Memerlukan Android
Android 4.1+
Category
Laporkan
Tafakari Injili
1.0 by AlberaInfoTech
Feb 20, 2022