Use APKPure App
Get Nuru AfyaCheck old version APK for Android
ہماری ایپ آپ کو حمل کی ترقی اور بچے کی نشوونما کو ٹریک کرنے دیتی ہے۔
NuruAfyaCheck ni application inayokupa taarifa na ushauri wa afya ya mama na mtoto kwa lugha ya Kiswahili. App yetu pia inakuwezesha kufuatilia maendeleo ya ujauzito na ukuaji wa mtoto.
MATUMIZI:
Kwa ujumla application ya NuruAfyaCheck inakuwezesha:
1. Kupata ushauri kwa makala na nyenzo mbalimbali kukusaidia kufanya "UZAZI WA MPANGO"
2. Kufuatilia maendeleo ya "UJAUZITO" wiki hadi wiki tangu kutungwa kwa mimba mpaka kujifungua.
3. Kufuatilia hatua za ukuaji na maendeleo ya afya ya "MTOTO" tangu kuzaliwa mpaka miaka mitano (5).
4. Kupata ushauri kwa makala na nyenzo mbalimbali kuhusu lishe kwa mama na mtoto.
KUJIUNGA:
Kujiunga ni rahisi sana. Utahitaji kupakua NuruAfyaCheck app na kujazaa taarifa kadhaa ilikujiunga. Baada ya kujiunga na kuingia ndani ya app (Login) utachagua huduma unayotaka kufuatilia, kisha utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa ufuatiliaji huduma husika.
Unaweza ukabadilisha taarifa za "Account" yako hapo baadae, ikiwemo kubadilisha huduma unayotaka kufuatilia kwa kubonyeza alama ya uso (face icon) iliyopo juu kabisa kulia kwenye app.
HAKI MILIKI:
Taarifa, Makala na Ushauri wowote uliopo kwenye NuruAfyaCheck app ni mali ya NuruFoundation. Kunakili, kuchapisha au kushirikisha wengine kwenye tovuti nyingine au mitandao ya kijamii bila kutushirikisha au kuomba idhini kutoka uongozi wa NuruFoundation ni kwenda kinyume na sheria zetu za haki miliki.
ANGALIZO:
Taarifa na maelezo yote yaliyopo kwenye app yasitumike kubatilisha au kama mbadala wa ushauri na huduma kutoka kwa mtaalamu toka kituo cha afya. NuruAfyaCheck chini ya Nuru Foundation inakutahadharisha kuwa haitahusika kwa namna yoyote ile na matokeo ya maamuzi yako utakayochukua kutokana na taarifa hizi zinazotelewa kama taarifa na ushauri kwa jamii yote kwa ujumla.
Taarifa na ushauri huu usitumike kama mbadala wa ushauri utakaopewa na daktari, mkunga au mtoa huduma kutoka kituo rasmi cha afya.
Kama una wasiwasi au tatizo kuhusu ujauzito au mtoto wako tafadhali wasiliana na daktari wako au mtoa huduma wa afya karibu yako.
Timu nzima ya NuruAfyaCheck inakutakia ujauzito mwema, kujifungua salama na malezi mema na afya bora kwako na kwa mtoto wako.
Last updated on Aug 17, 2021
Minor bug fixes and improvements. Install or update to the newest version to check it out!
Android درکار ہے
4.4 and up
کٹیگری
رپورٹ کریں
Nuru AfyaCheck
1.1.1 by Dephics Co. Ltd
Aug 17, 2021